Saturday, July 18, 2009

SWAHILI TEAM(Helsinki) imeifunga TAS(Tampere) 2-1

Wachezaji wa timu ya TAS wakiwa na mawazo kibao baada ya kipigo cha 2-1
Mashabiki wa timu ya wakenya kutoka Helsinki (swahili timu) wakisherekea ushindi wa tugoli tuwili kwa kamoja..aaa Namuona Paschal mwenye kofia shabiki number moja wa Swahili team.
Kapteni wa Tas alipomfunga kwa penalt kipa wa Swahili team.Yaani kipa aliona akiufwata itakuwa kifo akaona bora aende mmdogo mdogo kama anabanjuka..

Mwamuzi wa mchezi huo ambaye aliumudu vema mchezo na aliukamilisha kwa kwa kuwa zawadia wachezaji wawili kadi za njano na mmoja kadi ya valentine(red)..

Leo timu ya inayoundwa na wakenya yenye maskani yake jijini Helsinki imefanikiwa kuwafunga kwa taaabu sana timu Tampere Africans Sports (TAS) goli 2-1.

Mchezo ulikuwa mzuri mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilikuwa sare bila kufungana.Kipindi pili kenya walifanikiwa kutumia nafasi walizopata na kupiga magoli mawili ya haraka haraka.Mpaka mwisho wa mchezo.Swahili Team 2-1Tas.

Mchezo ulimalizika kwa wachezaji pamoja na watazamaji kupata msosi mzito pamoja na vinywaji ili kuitimisha siku.

Tutafika tu.

NGOMA AFRICA WATUA UFINI

Kiongozi wa Ngoma Africa ,Ras Makunjabaada ya kushuka kwenye liusafiri akitokea uwanja wa ndege wa jiji la Tampere.

Lile kundi l The Ngoma Africa Band wamewasili jijini tampere kutumbuiza kwenye tamasha kubwa la Fest Afrika

Ras Makunja ambaye hakuwa na mengi ya kusema zaidi ya kuhaidi kutoa burudani kubwa kama ilivyo desturi ya bendi hiyo.

Picha za tamasha ilo ambalo litafanyika leo zitawajia muda si mrefu..Blog yenu itakuwepo kuwaletea matukio FASTA FASTA..

Tutafika tu

Thursday, July 9, 2009

MSAADA KWA BLOG YA MAGAZETI


Mdau mkubwa anayeendesha blog ya magazeti ya tanzania katika kuhabarisha dodosa za magazeti mbalimbali ya nyumbani Tanzania Kennedy Kimaro anaomba msaada mwenye taarifa ya jinsi atavyoweza kupata Professional Macro Lens for Kodak EasyShare Z650.

Unaweza kuwasiliana na Kennedy kupiti
Kennedy Kimaro
P.O Box 347,Dsm-Tz
Mob:+255 784 247723
E-mail: kimarokennedy@hotmail.com au
mbezisokini@gmail.com



Kumradhi:Nimerejea sasa

Natumia mwanya huu kwa ndugu zangu wote ambao umekosa mtundiko kwa siku kadhaa.Hii ilitokana na hali ngumu ya kiuchumi "risesheni" ila sasa naona mambo yakuwa mswano.

Tutpo pamoja tuendeleze safari yetu...


Tutafika tu

Monday, June 29, 2009

NGOMA AFRIKA AFRIKA WAENDELEZA MATAMASHA ULAYA

Kiongozi wa Ngoma Africa Band Ras Makunja

The Ngoma Africa Band aka FFU!na mdundo wao wa "Bongo Dansi" wanatarajiwa kutingisha jukwaa lingine katika onyesho kubwa la Afrika Festival litakalo fanyika mijini Goeppingen,Ujerumani siku ya jumamosi ya 4 Julai 2009 saa 2.00 Usiku.

Bendi hiyo maarufu na dansi lake linalowatia kiwewe washabiki huko ughaibuni, wanasubiliwa kwa hamu na washabiki katika onyesho hilo.Wasikilize hapa
pia unaweza kuwasiliana kwa kupitia

Saturday, June 27, 2009

KILI FC(Sweden) waendeleza UBABE FINLAND

Wachezaji Kilimanjaro Fc kutoka sweden wakiserebuka baada yakuwabamiza bila huruma timu ya mpira ya wabongo yenye maskani yake jijini Helsinki kwa mabao 8 kwa kamoja.
Kwisha stori:wapo hoi wamekata tamaa mpira umekwisha wameshapewa bilauli 8 za maji.Msijali mpira unadunda.(Picha zote kutoka kwa mdau George Matovu-Mtv)

Kilimanjaro Fc kutoka sweden imeendeleza ubabe kwa kuibanjua Bongo Fc nyumbani kwao Heslinki magori 8-1.

Bongo Fc walionekana kuzidiwa kimchezo,mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Kilimanjaro FC walikuwa wanaongoza kwa magoli 5 kwa nunge.Kipindi cha pili Bongo Fc walifanikiwa kujipatia kagoli kakufutia macho.

Mpaka mwisho wa mtanange,Kili Fc 8 na ndugu zao Bongo Fc 1.
Kilimanjaro Fc wameibugiza bongo fc magoli 8-1 

Ikumbukwe mara ya mwisho walikutana mwaka jana Sweden na Kilimanjaro kuibuka washindi 4-3.

Pongezi sana Kilimanjaro Fc kwa ushindi mnene.Poleni sana majirani Bongo Fc kwa kichapo cha mwaka...aaa aa

Tutafika tu

Thursday, June 25, 2009

Hasheem Thabit SAFIRINI NBA

Hasheem Thabit mtanzania ambaye anapewa nafasi kubwa ya kupata nafasi ya kihistoria katika medani ya mpira wa kikapu kucheza ligi kubwa duniani na kuwa mchezaji wa kulipwa.

Kila la kheri dua zetu tupo nawe ufanikiwe kufanya vema na kuzidi kupeperusha vema bendera ya nchi yetu.

Kila la kheri Hashem natumaini utapita mkubwa.

Maelezo zaidi kuhusu Hasheem na mchujo huo unaweza kutembelea hiyo linki 2009 NBA Draft




Tutafika tu.